Search This Blog

Tuesday, May 18, 2021

Jaji Mkuu Sudan afutwa kazi,mwendesha mashtaka mkuu ajiuzulu


Sudan imetangaza kujiuzulu kwa mwendesha mashtaka wake mkuu na kumtimua jaji mkuu wa mahakama.

Baraza kuu linaloongoza nchini humo Jumatatu lilisema kwamba limekubali kujiuzulu kwa Tajalsir al-Hibir, mwendesha mashtaka wa umma, ambaye alikuwa amewasilisha kujiuzulu kwake mara kadhaa huko nyuma.

Hakuna sababu zilizotolewa za maamuzi hayo - ambayo yalikuja baada ya baraza hilo kuamuru uchunguzi ufanyike wiki iliyopita wa mauaji ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi huko Khartoum.

Watu wengi nchini Sudan pia wamekuwa wakidai haki kwa makumi waliouawa wakati wa maandamano mnamo 2019 ambayo yalisababisha kuondolewa madarakni kwa Rais Omar al-Bashir.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...