Search This Blog

Saturday, May 29, 2021

Mahakama ya Mali yamtangaza Goita kuwa rais wa mpito

 


Mahakama ya Katiba ya Mali imemtangaza Kanali Assimi Goita, ambae aliongoza mapinduzi ya kijeshi ya juma hili ya taifa hilo la afrika magharibi kuwa rais wa mpito. Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema Goita anapaswa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Rais Bah Ndaw ambaye amejiuzulu. 


Uamuzi huo unazidisha mkwamo ambapo viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wapo katika maandalizi ya kukutana kesho kuzungumzia hatua ya kukabidhi madaraka, ambayo inahatarisha harakati za kuelekea kwenye demokrasia na kudhoofisha mapambano dhidi ya waasi. 


Rais Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane walijiuzulu nyadhfa zao baada ya kuwekwa kiuzizini kwa siku kadhaa juma hili, katika mapinduzi ambayo yanatajwa kupangwa na Goita, ambae alijitangaza kuwa rais mara moja.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...