Search This Blog

Saturday, May 29, 2021

Karibu watu 400,000 nchini DRC wamekimbia kwa hofu ya kuripuka tena volcano


Takriban watu 400,000 wameukimbia mji wa Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya serikali kutoa onyo la kuripuka tena kwa volkano katika Mlima Nyiragongo.


Maafisa wa Goma wamesema familia 80,000 ambazo ni sawa na watu 400,000 waliondoka Goma siku ya Alhamisi baada ya amri ya jitihada ya tahadhari kutolewa na serikali.Serikali ya Congo inafanya juhudi za kutoa misaada ya maji ya kunywa, chakula na vifaa vingine na wafanyakazi wanasaidia kuwakutanisha watoto waliotengana na familia zao. 


Awali, ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kiutu, OCHA ilikadiria kuwa takriban watu 400,000 kati ya 600,000 wa mji huo wataathirika na agizo hilo ambalo limetolewa kwenye wilaya 10 kati ya 18. Watu 34 wamekufa kutokana na athari za mripuko huo wa volkano wa juma lililopita.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...