Search This Blog

Wednesday, May 26, 2021

Biden na Putin wamekubaliana kukutana Juni

Rais wa Marekani Joe Biden na wa Urusi Vladimir Putin wamekubaliana kukutana mwezi ujao mjini Geneva. 

Mkutano huo wa ana kwa ana unatarajiwa kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya viongozi hao wawili ambao umezidi kuwa mbaya tangu Biden kuingia madarakani. 

Mkutano huo wa Juni 16 utafanyika mwishoni mwa ziara ya kwanza ya Biden ya kimataifa. Biden pia ataitembelea Uingereza na kushiriki mkutano wa Kundi la nchi saba tajiri ulimwenguni pamoja na kuhudhuria mkutano wa NATO mjini Brussels.

 Ajenda ya mazungumzo inatarajiwa kujumuisha majadiliano juu ya hatua za Urusi katika nchi jirani ya Ukraine, tukio la wiki hii nchini Belarus, pamoja na juhudi za mataifa yote mawili za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...