Benki ya Dunia imesema imeipatia serikali ya mpito ya Sudan dola bilioni 2 kuisaidia kutatua matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba nchi hiyo kwa miongo kadhaa.
Fedha hizo zitatumia kufadhili miradi mikubwa ya kujenga miundombinu, pamoja na kuwasaidia watu waliopoteza makazi yao, amesema Hafez Ghanem Makamu wa rais wa Benki ya Dunia wa eneo la mashariki na kusini mwa Afrika.
Aliyasema hayo akiwa mjini Khartoum hapo jana, ambapo alikutana na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na Waziri wa Fedha Gibril Ibrahim, kulingana na ofisi ya waziri mkuu.
Benki ya Dunia imechukua hatua hiyo baada ya Sudan kulipa madeni yake iliyokuwa ikidaiwa kwa msaada wa Marekani wa dola bilioni 1.15.
Ghanem amesema jumuiya ya kimataifa imefurahishwa na juhudi za serikali ya Sudan za kukuza uchumi na kupambana na umasikini pamoja na kuanza mageuzi muhimu ya kiuchumi.

No comments:
Post a Comment