Search This Blog

Tuesday, May 25, 2021

Imefika muda muafaka wa kumletea Jaden mdogo wake- Ray

 


Muigizaji nguli wa filamu nchini Vicent Kigosi 'maarufu kama Ray' atamani kupata mtoto mwengine, mwanae Jadent\ apate mdogo wake.

Ray ameeleza hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo anadhani ni muda sahihi sasa, na kwa uwezo wa Mungu hakuna kinachoshindikana.

"Tunaishi Dunia yenye watu wanao tisha ambao hata hauwezi kuamini kama nao ni Binadamu wenzako. Pamoja na hayo usikubari kukatishwa tamaa na watu hao, tambua kuwa yupo Mungu anayekupenda kuliko unavyoweza kuelewa na Mungu huyu ana mpango wa Ajabu kwaajili ya Maisha yako.

Mengi yalisemwa juu yangu lkn leo nami naitwa Baba na kijana wangu Kipenzi @jadenthegreatest asante Mungu kwa zawadi hii hakika sasa umefika muda muafaka kwa uwezo wako kuleta mdogo wake na Jaden hakika kwa uwezo wako hakuna kitakacho shindikana'' - ameandika Ray.

Mtoto wa kwanza wa Ray ambaye ni Jaden alifanikiwa kumpata na msanii mwenzake Chuchu Hansy.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...