Brussels,Bunge Ulaya limepitisha sheria itakayolazimishwa kuondolewa ndani ya saa moja baada ya kugundulika kwa ujumbe wowote wenye maudhui ya propanda za kigaidi katika tovuti.
Hatua ya kupigia kura sheria hiyo, ndio ya mwisho inayohitajika katika kuifanya sheria hiyo ifanye kazi, ingawa mchakato wake haujakamilika kuifanya ifanye kazi mara moja.
Kimsingi sheria hiyo itazihusu nyaraka zitakazochapishwa katika eneo zima la Umoja wa Ulaya.
Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya kutoka Poland Patryk Jaki, amesema sherian hiyo takuwa nyenzo muhimu na kudhihirisha kwa namna gani mara nyingi mtandao wa internet unatumika na magaidi katika kusambaza ujumbe wao.
Hatua hiyo inatokana na maridhianon wabunge na wawakilishi wa mataifa ya Desemba mwaka jana.

No comments:
Post a Comment