Search This Blog

Thursday, April 29, 2021

Benki ya dunia imetoa kiasi cha dola milioni 100 kwa eneo tete la kaskazini mwa Msumbiji

 


Pemba, Benki ya Dunia dunia hapo jana imetoa kiasi cha dola milioni 100, kama fedha za dharura kwa shabaha kurejesha hali ya kawaida katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji, ambako maelfu ya watu wameachwa bila ya makazi kutokana na vurugu za makundi ya wenye itikadi kali.

Makubaliano ya fungu hilo, ikiwa kama sehemu ya makubaliano ya mradi wa miaka mitatu utakaogharimu milioni 700, umetiwa saini kwa upande moja na serikali na mwingine ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ufuatiliaji wa mradi husika ijulikanayo kama UNOPS.

Rais Filipe Nyusi ambae alihudhuria hafla ya utiaji sani mjini Pemba, alisema makubaliano hayo yatasaidia kutatua janga la kibinaadamu.

Eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi la jimbo la Cabo Delgado limekumbwa na matukio ya umwagikaji damu tangu mwaka 2017, kunakodaiwa kufanwa na kundi la al-Shabaab. 

Katika tukio la Machi 24 lenye kuhusisha kundi hilo katika mji wa Palma idadi kubwa ya watu waliuwawa na wengine zaidi ya 25,000 kugeauka kuwa wakimbizi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...