Ujerumani na China hapo jana zimekubaliana kuongeza ushirikiano wao katika kukabiliana na kadhia ya mabadiliko ya tabia nchi.
Lengo ni kudhibiti kasi ya ongezeko la kiwango cha joto duniani ambacho kinakadiriwa kuwa cha zaidi ya nyuzi joto 1.5 kinyume na malengo yaliyopo.
Waziri wa Mazingira ya Ujerumani, Svenja Schulze, amesema wanapaswa kufanya kila liwezekanalo katika kukabiliana na kupunguza hewa chafu katika uso wa dunia kwa kiasi kikubwa kuliko hata ilivyopangwa hapo awali.
Wanasayansi wanasema hata kabla ya zama mapinduzi ya viwanda, tayari kiwango cha joto kilikuwa kimeongezeka kwa nyuzi joto 1.2.
Na kwamba jumuiya ya kimataifa imeshindwa kukabiliana na kupunguza kiwango hicho kwa zingatio la makubalino ya mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris, ambao uliridhiwa miaka mitano iliyopita nchini Ufaransa.
China kwa sasa ndio taifa lenye kuchangia uchafunzi mkubwa wa mazingira kwa sasa duniani, ikiwa imeipiku Marekani yenye kushika nafasi ya pili.

No comments:
Post a Comment