Search This Blog

Tuesday, April 27, 2021

Marekani na Uingereza kuisaidia India katika vita dhidi ya Covid-19

 


Marekani na Uingereza zimechukua hatua ya haraka za kuisaidia India mashine za kupumulia na vifaa vya chanjo, baada ya hali ya taifa hilo kuelezwa na Shirika la Afya Duniani kuwa mbaya zaidi, huku Italia ikianza kuondosha vizuizi vya kukabiliana na janga la Covid-19.

India yenye idadi ya watu bilioni 1.3, inapambana na ongezeko kubwa la maambukizi, na hospitali zimezidiwa ambapo pia vituo vya kuchoma maiti kama utaratibu wa mazishi ya Kiindi, vinafanya kazi hiyo kwa wakati wote.

Kwa rekodi za jana Jumatatu kwa mfano, kumekuwa na maambukizi mapya 352,991 na vifo 2,812. Kiwango hicho kikitajwa cha juu zaidi kuwahi kutokea tangu kuzuka kwa janga la virusi vya coroa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO, amesema kutokana na hali ilivyo shirika hilo linafanya pia kila linalowezekana katika kusambaza vifaa muhimu na nyenzo nyingine katika kuwanusuru raia.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...