Search This Blog

Tuesday, April 20, 2021

Rais wa China asema ulimwengu unahitaji usawa na sio utawala wa kundi moja kwa jengine

 


Rais Xi Jinping wa China amesema mfumo wa utawala wa kilimwengu lazima ufanywe uwe wa usawa na uadilifu zaidi, na kwamba kanuni zinazowekwa na nchi moja ama baadhi ya mataifa haziwezi kulazimishwa kufuatwa na wengine. 

Akizungumza hivi leo kwenye Jukwaa la Boao kwa Asia, rais huyo wa taifa la pili kwa nguvu ulimwenguni amesema dunia inahitaji zaidi haki na sio utawala wa kundi ama nchi moja. 

Xi amewaambia washiriki wa jukwaa hilo, ambalo ni sawa na jukwaa la uchumi la Davos, kwamba kujenga vizuizi na kulazimisha mgawanyiko kutawaumiza watu wote na kamwe hakufaidishi hata mmoja. 

Bila ya kulitaja taifa lolote kwa jina, Rais Xi amesema kuwa dunia ya sasa inapaswa kukataa kurejea kwenye zama za vita baridi, huku akisema China itaendelea kupunguza orodha aliyoiita 'hasi' kwa ajili ya uwekezaji wa kigeni.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...