Search This Blog

Tuesday, April 20, 2021

Marekani yaonya hatua ya Urusi kuweka vizuizi kwenye Bahari Nyeusi

 


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeionya Urusi dhidi ya kile inachosema ni "uchokozi usio sababu", baada ya Urusi kutangaza mipango ya kuweka vizuizi kwenye sehemu ya Bahari Nyeusi, ambavyo vinaweza kuathiri njia za kuzifikia bandari za Ukraine. 

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Ned Price, inasema hatua hiyo ni ishara ya kuendelea kwa kampeni za kuihujumu Ukraine. 

Vyombo vya habari vya serikali nchini Urusi viliripoti kuwa serikali inadhamiria kuzifunga baadhi ya sehemu za bahari hiyo kwa meli za kijeshi na serikali za kigeni kwa miezi sita. 

Ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, itazuwia kuzifikia bandari za Ukraine kwenye Bahari ya Azov, inayoungana na Bahari Nyeusi kupitia Mlango Bahari wa Kerch, mashariki mwa Rasi ya Crimea, iliyotwaliwa na Urusi mwaka 2014.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...