Search This Blog

Tuesday, April 20, 2021

Armin Laschet achaguliwa kumrithi Merkel

 


Muungano wa vyama vya kihafidhina nchini Ujerumani umemchaguwa kiongozi wa chama cha Kansela Angela Merkel, CDU, kwa wingi mkubwa kuwa mgombea wa ukansela kwenye uchaguzi mkuu ujao.

 Baada ya masaa zaidi ya sita ya mazungumzo, baraza kuu la chama hicho lenye wajumbe 46 lilipiga kura ya siri ya mtandaoni, ambapo asilimia 77.5 zilimuunga mkono waziri mkuu wa jimbo lenye watu wengi la Northrhine Westphalia, Armin Laschet. 

Mpinzani wake, Markus Soeder, ambaye ni waziri mkuu wa jimbo tajiri la Bavaria na kiongozi wa chama ndugu cha CSU, alipata asilimia 22.5. 

Tangu awali, Soeder, ambaye ni maarufu zaidi kwenye kura za maoni kuliko Laschet, alikuwa ameshasema kwamba angelikubaliana na uamuzi wa CDU na kujitowa kwenye kinyang'anyiro hicho bila kinyongo. 

Kura hiyo ya usiku wa kuamkia leo imehitimisha wiki kadhaa za kile kilichoonekana kama vita vya madaraka vya kumrithi Kansela Merkel.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...