Cuba imehitimisha enzi za utawala wa familia ya Castro na kuanza zama mpya, baada ya hapo jana chama tawala cha kikomunisti kumchaguwa Rais Miguel Diaz-Canel kuchukuwa nafasi ya Raul Castro kama mkuu wa chama hicho.
Hata hivyo, Diaz-Canel, ambaye alirithi nafasi ya urais mwaka 2018, ameahidi kuendelea kutaka ushauri wa mtangulizi wake kwenye maamuzi ya kimkakati.
Ukabidhianaji huo wa madaraka unaashiria mwisho wa miongo sita ya utawala wa ndugu wawili, Fidel na Raul Castro, ambao waliongoza mapinduzi ya 1959 kwenye taifa hilo la Caribbean lenye raia milioni 11, na kuanzisha mfumo wa kikomunisti mbele ya mlango wa Marekani.
Diaz-Canel, mwenye umri wa miaka 60, aliwahi kuwa mkuu wa chama hicho kwenye majimbo mawili, kabla ya kujiunga na serikali kuu mwaka 2009.

No comments:
Post a Comment