Search This Blog

Monday, April 26, 2021

Nataka kuinunua Arsenal - Daniel EK

Mwasisi na Afisa mtendaji mkuu wa mtandao wa Spotify ambao unajihusisha na biashara ya muziki ya mtandaoni amekiri kuwa tayari kuinunua klabu ya Arsenal kama familia ya Kroenke ipo tayari kuiweka sokoni.

Daniel ameyasema hayo kupitia akaunti yake ya Twitter wikiendi hii baada ya kuwepo na mgomo mkubwa wa mashabiki wa Arsenal kushinikiza wamiliki hao wajiondoa baada ya kutoona mafanikio uwanjani pamoja na kukubali kusaini mkataba na kushiriki European Super Ligi.

Daniel ameandika, “Tokea utotoni, nimekuwa nikiifurahia Arsenal. Kama Kroenke angependa kuiuza Arsenal basi nitakuwa na furaha kubwa ya kutaka kuinunua.”.

Tajiri huyo raia wa Sweeden ni miongoni mwa wafanyabiashara maarufu duniani na mwenye ushawishi kama ilivyothibitishwa na jarida la Billborad la Marekani pamoja na kuwa na utajiri unaokadiriwa kufika paundi bilioni 3.3 za Entgland ambazo ni zaidi ya Trilioni 1 na zaidi ya milioni 400.

Daniel amesema kama wazo lake hilo litafanikiwa basi angependa kushirikiana na baadhi ya magwiji wa Arsenal, Dennis Bergkamp, Thierry Henry na Patrick Vieira ili iwe rahisi kufabikiwa klabuni hapo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...