Paris St-Germain wapo mbele ya Manchester United katika harakati za kumsajili mshambuliaji nyota wa Ureno na Juventus, Cristiano Ronaldo, 36. (Tuttosport - in Italian)
Manchester United wanamuwinda mshambuliaji wa klabu ya Slavia Prague's Msenegali Abdallah Sima, 21. (Manchester Evening News)
RB Leipzig wanataka dau litakalovunja rekodi la usajili wa makocha la Euro milioni 25 kutoka Bayern Munich ili kumuachia kocha wao Julian Nagelsmann (Sky Sports)
Klabu ya Tottenham sasa itaaelekeza nguvu kumsajili kocha wa Ajax Eric ten Hag, wakati huu ambapo Bayern inaonekana ipo mbioni kumsajili Nagelsmann. (Telegraph)Golikipa Mtaliano Gianluigi Donnarumma, 22, atasalia klabuni AC Milan licha ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu na kutakiwa na na klabu za Manchester United na Chelsea. (TalkSport)
Real Madrid hawatakaza msuli kumbakisha klabuni hapo beki wa Ufaransa Raphael Varane, 28, ambaye amekuwa akiwaniwa na Manchester United na Chelsea. (AS - in Spanish)
Kiungo wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 29, anataka kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu ili kupata sehemu atakayocheza zaidi. (Football Insider)
Arsenal wameanzisha mazungumzo na kiungo wao kinda Emile Smith Rowe, 20, ili kumpatia mkataba mpya. (The Athletic - subscription required)
Arsenal ipo tayari kuwauza wachezaji wanne mwishoni mwa msimu ili wapate fedha za kufanya usajili. (Football London)
Chelsea na Manchester United wanamuwinda kiungo kinda wa Brighton' Andrew Moran, 17. (Team Talk)
Barcelona wanaimani kuwa Eric Garcia, 20, atajiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wa beki huyo na klabu yake ya Manchester City. (Mundo Deportivo - in Spanish)
AS Roma imemchagua kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus Maurizio Sarri kuwa mkufunzi wao mara baada ya msimu huu kukamilika. (Corriere dello Sport - in Italian





No comments:
Post a Comment