Serikali mpya ya mpito nchini Chad imemtaja waziri mkuu wa zamani Albert Pahimi Padacke kuwa waziri mkuu wa mpito.
Pahimi Padacke alikuwa waziri mkuu chini ya serikali iliyopita ya Rais Idriss Deby, ambaye kifo chake cha ghafla kimesababisha kuundwa kwa serikali ya kijeshi ya mpito inayoongozwa na mtoto wake Mahamat Idriss Deby.
Pahimi Padacke anatarjiwa kuongoza serikali ya mpito mbayo wajumbe wake watatajwa ama kuondolewa na kiongozi wa serikali hiyo, hii ikiwa ni kulingana na amri iliyotolewa na serikali.
Baraza la kijeshi lilichukua madaraka mwishoni mwa wiki, na kuahidi kufanya uchaguzi baada ya miezi 18.

No comments:
Post a Comment