Search This Blog

Friday, April 23, 2021

Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii baraza la wawakilishi asema haya kuhusu mradi wa Viungo


Na Thabit Madai,Zanzibar.

MWENYEKITI  wa kamati ya kilimo biashara na utalii kutoka Baraza la wawakilishi Ali Suleiman Ameir amesema wakati utekelezaji wa mradi wa viungo ukiendelea kuna haja watendaji kuhakikisha wanafanya kazi hio kwa moyo wa uzalendo ili uweze kuleta tija zaidi kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.

Aliyasema hayo wakati wa kikao maalumu katika ofisi za utekelezaji huo Mwanakwerekwe mjini Unguja kufuatia kikao kilichokua la lengo la majadiliano ya kufanya ushawishi wa kisera kuhusu sekta  ya kilimo.


Alisema wakati mradi huo unatekelezwa watendaji wanapaswa kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha wanapata matukio chanya ya mradi huo kinyume na miradi mengine ambayo imeshindwa kufanya vizuri.

Pamoja na hayo alisema ipo haja kuhakikisha kuwa wanufaika wa mradi huo ni walengwa husika na sio watu wengine kwa lengo la kuondoa chanagamoto mbali mbali.

‘’Lazima tutambue kuwa jamii na Serikali kwa ujumla ina matumaini makubwa na mradi huu kwa maslahi ya wananchi wake hivyo lazima mufanye kazi kwa umakini sana’’aliongezea.

Kwa upande wake mtalamu wa maswala ya kilimo Salum Rehani alisema ipo haja kwa Serikali kuweka utaratibu maalumu wa utafiti ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutambua mbegu bora za kilimo zinazopaswa kupandwa kulingana na mazingira husika.

Alisema kwa mara kadhaa Serikali imekua ikipoteza gharama kubwa ya fedha kwa kununua mbegu pamoja na mbolea lakini matukio yake faida inayopatikana haiendani na uhalisia kutoka na hasara mbali mbali wanazokutana nazo wakulima.

‘’Ninaamini kuwa iwapo utafiti utafanyika tutakua na uhakika tunalima bidhaa gani,wapi na kwa muda gani na sio watu kukurupuka tu kwa mfano unaona jinsi zao la nyanya linavoshuka bei kwa kuwa watu wote wanalima wakati mmoja’’aliongezea.

Kwa upande wake Meneja wa utekelezaji mradi huo kanda ya Unguja Bi Khadija Juma alisema Zanzibar ni sehemu iliojaliwa na fursa kubwa katika sekta ya kilimo na kwamba anaamini utekelezaji huo utaleta faida chini ya mashirikiano ya pamoja.

Aidha Meneja huyo  hayo aliwaomba wajumbe wa Baraza la wawakilishi kuendelea kuishawishi Serikali kutambua umuhimu wa kuekeza zaidi katika kilimo kwani kilimo ni sekta muhimu kwa maslahi ya Taifa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...