Search This Blog

Friday, April 23, 2021

Waziri wa Elimu asema ataendelea kutekeleza maagizo 15 ya Rais


Na Thabit Madai, Zanzibar. 

WAZIRI  wa Elimu na Mafunzo ya  Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said amesema Wizara yake inaendelea kutekeleza maagizo 15 ya Rais wa Zanzibar na Mwenyeketi wa baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati alipowaapisha Mawaziri wake.

Amesema katika masuala ya kiwa.wabunifu Wizara yake imechukua hatua kuwatafuta wataalamu wa ujenzi wa.madarsa kwa kutumia kuta maalum ili kupunguza tatizo la utegemezi wa mchanga.

Akizunguza katika Skuli ya Msingi na Sekondari Mbuzini wakati alipofika pamoja na Viongozi wa Wizara hiyo, kuangalia mfano wa darasa lililojengwa kwa kutumia kuta, mhe Simai amesema pamoja na kuwa tatizo la mchanga limetatuliwa, lkn  ni vyema kuangalia na uwezekano mwengine wa ujenzi kwa.kutumia kuta ili kupunguza gharama.

Amesema lengo la Serikali ni kujenga Skuli za ghorofa ili kusaidia kupunguza msongamano  wa wanafunzi  darasani, lakini kutokana hali ya kifedha ilivyokuwa ni ndogo, ujenzi wa darasa kama hilo  unaweza kujengwa kwa muda mfupi iwapo wahandisi wa Wizara watathibitisha kuridhika na viwango vya ujenzi wa darasa hilo na utaweza kusaidia kupunguza.gharama za ujenzi na hivyo kusaidia katika kupunguza msongamano wa wanafunzi Madarasani.

Aidha mhe Simai amefahamisha kuwa katika suala la ujenzi hakuna mbadala wa tofali lakini pia inaonekana kuwa na woga katika kutumia teknolojia, hivyo amesema katika wizara yake hawatokuwa na woga na wataendelea kuwa na ubunifu katika kutumia teknolojia mbalimbali kwa lengo la kuleta manufaa mema na mabadiliko katika sekta ya elimu.

Hata hivyo mhe Simai amesema kabla ya kulikubali darasa hilo, watawaita viongozi husika kwa lengo la kulikagua na kupata ridhaa, kwa.lengo lile lile la Serikali kuhakikisba watoto wanasoma katika mazingira bora na salama.

Nae Mkurugenzi wa kampuni ya (Prefam Industries) inayojishughulisha na ujenzi kwa kutumia kuta, ambayo imejenga darasa hilo bwana Taufiq Iddi Taufiq amesema juhudi hizo zinatokana na kuunga mkono Serikali iliyopo madarakani katika kuleta ubunifu katika masuala ya ujenzi na kuondoa changamoto ziliopo hasa katika masuala ya mchanga.

Amesema ujenzi wa darasa hilo ni nafuu na umejengwa kwa  kuzingatia viwango vyote vya ujenzi vya Wizara katika ujenzi wa darasa, pamoja na usalama wa watoto na ubora kwani unasaidia kupunguza joto kutokana na malighafi zilizotumika ndani yake.

Amesema kwa Zanzibar ni Teknolojia hiyo ni mpya ambayo ndio wanaitangaza sasa, lakini tayari wameshajenga nyumba nyingi za makaazi Dar ess Salaam na hawajapata malalamiko ya aina yeyote.

Amesema utaratibu wa kutunza  unapaswa kuwepo kama yanavyotunzwa majengo mengine, ingawa ujenzi wake ni nafuu sana na wa haraka ukilinganisha na ujenzi wa kutumia mafofali.

Aidha ameiomba Wizara ya Elimu na Wizara nyengine kuangalia uwezekano wa kuanza kutumia Teknolojia hiyo kwani ni rahisi, haraka na salama.

Kwa upande wake Mhandisi wa Wizafa ya Elimu ndugu Salum Ali Juma ameshukuru kupewa teknolojia hiyo mpya ambayo imejengwa kwa Gharama nafuu na haraka, ambapo amempongeza mhe Waziri kwa hatua aliyoichukua ya kuweza kikabiliana na tatizo la mchanga.

Amesema kikawaida ujenzi wa darasa hilo hutumia gari sita za tani 10 za mchanga lakini kwa kutumia bidhaa za (Prefam) ujenzi wa darasa hilo umetumia gari moja tu ya tani 10 ya mchanga ambapo gharama zake kwa kutumia tofali zao za kongriti wanagharimu darasa hilo shilingi milioni 28 mpaka kumalizika kwake, lakini kwa kutumia vifaa vya (prefam) wameweza kutumia shilingi milioni 16 mpaka kumalizika kwa darasa hilo.

Aidha amesema  wanategemea kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo ZBA endapo watahibitisha ubora.wa darasa hilo wanaweza kuitumia geknolojia hio.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...