Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.Image caption: Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.
Kampuni yenye makao yake nchini Lesotho imeruhusiwa kukuuza mazao ya bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.
Kampuni hiyo kwa jina, MG Health, imesema Alhamisi kwamba imepokea uthibitisho rasmi kwamba mchakato wake wa utengenezaji unakidhi viwango vya uzalishaji vya Muungano wa Ulaya.
Kampuni hiyo inakuwa ya kwanza barani Afrika kuuza bangi kwa ajili ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.
"Kile ambacho hii inamaanisha ni kwamba tuna idhini ya kuuza bidhaa zetu kama API [ kiungo cha kifamasia] ndani ya Ujerumani, na soko pana la Muungano wa Ulaya . Tunatarajia kuanza mwezi Juni ," Shirika la habari la Reuters lilimnukuu Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Andre Bothma akisema.
Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea kutoka London, alikokuwa amesafiri kufanyiwa kimatibabu.
Kurudi kwake siku ya Alhamisi kulitangazwa kupitia ujumbe wa akaunti ya Twitter ya serikali:
Rais, ambaye alifanya ziara ya ‘kawaida ya matibabu’ kwenda Uingereza mnamo Machi 30, amekosolewa sana kwa kuamua kutibiwa nje ya nchi wakati mfumo wa huduma ya afya nchini mwake ‘ukisimamiwa vibaya na kukosa ufadhili wa kutosha’vyombo vya habari vya huko viliripoti,Nigeria pia inakabiliwa na ukosefu wa usalama, huku mashambulizi kadhaa yakiripotiwa wakati Rais Buhari alipokuwa hayupo

No comments:
Post a Comment