Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ametibiwa hospitalini baada ya kuugua malaria wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa na Gabon.Mchezaji huyomwenye umri wa miaka 31 alifunga katika ushindi wao wamabao 3-0 wa Gabon dhidi ya DR Congo katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa bingwa Afrika mnamo Machi 25.
Aliichezea Arsenal katika mchuao wao wa kombe la bara Uropadhidi ya Slavia Praguetarehe 8 Aprili lakini akosa mechi walioishinda Sheffield United Siku ya Jumapili
" Nimekuwa hospitalini kwa siku chache wiki hii’ alisema kupitia Instagram
" Ninahisi nauu kila siku kwa hisani ya madaktaru borawaliogunduana kunitibu haraka’

No comments:
Post a Comment