Mkurugenzi wa Kituo cha Kiafrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Daktari John Nkengasong, alitangaza kuwa wanapinga wazo la "pasipoti ya chanjo" kwa sababu ya shida zinazokabiliwa na nchi masikini katika kupaikanaji wa chanjo ya corona (Covid -19).
Nkengasong alitoa maelezo katika mkutano wa kila wiki wa waandishi wa habari mtandaoni na kusema kwamba nchi za bara hilo hazina chanjo za kutosha, na kwamba nchi tajiri zilizo na chanjo hazitakuwa sahihi kuweka vikwazo vya usafiri kwa raia wa nchi zingine.
Nkengasong aliongezea kusema,
"Matumizi yoyote ya pasipoti za chanjo yatasababisha ukosefu wa haki wa hali ya juu."
Kwa upande mwingine, Nkengasong alitangaza kuwa nchi kama vile Shelisheli na Mauritius katika bara hilo zimepata chanjo inayohitajika kwa kinga ya kijamii.
Msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Margaret Harris, alitoa maelezo mnamo Aprili 6 na kusema kwamba bado hawajakaribisha "pasipoti ya chanjo" kwa sababu ya kutokuwa na uhakika kuhusu iwapo chanjo zinazuia usambazaji wa virusi na kama bado kuna ukosefu wa haki katika usambazaji wa chanjo ulimwenguni.

No comments:
Post a Comment