Search This Blog

Friday, April 9, 2021

Kiongozi wa Udugu wa Kiislamu Misri jela maisha


Mahakama nchini Misri jana imemuhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa kundi la Udugu wa Kiislamu Mahamoud Ezzat. 

Taarifa hii ni kulingana na gazeti linalomilikiwa na serikali la Al-Ahram. Ezzat alikuwa akikabiliwa na madai ya ugaidi yanayohusiana na machafuko ya baada ya jeshi kumuondoa madarakani rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi, Julai, 2013.

Ezzat alikamatwa mjini Cairo Agosti mwaka jana, na polisi walidai kumkuta na kifaa cha mawasiliano ambacho hakiwezi kuingiliwa alichokitumia kuwasiliana na wanachama wengine wa kundi hilo wa ndani na wa nje ya Misri. 

Alikutwa pia na hatia ya kusambaza silaha wakati wa mapigano kati ya wafuasi wa Udugu wa Kiislamu na wapinzani wao. 

Aidha, alikabiliwa na madai ya kuhusika na mauaji ya mwendesha mashitaka wa zamani Jenerali Hisham Barakat, aliyepinga vuguvugu la Udugu wa Kiislamu, mnamo mwaka 2015.

Wakili wake bado hajazungumzia chochote kuhusiana na kifungo hicho.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...