Search This Blog

Friday, April 9, 2021

Ufilipino na Marekani wahofia meli za China


Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken pamoja na mwenzake wa Ufilipino Teodoro Locsin kwa pamoja wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na boti za wanamgambo wa China zilizoko katika bahari ya China Kusini. 

Mawaziri hao wameelezea wasiwasi huo kwenye mazungumzo yao kwa njia ya simu.Ufilipino imeelezea uwepo wa mamia ya boti hizo za China ndani ya eneo la maili 200 za ukanda maalumu wa kiuchumi kwenye Bahari ya China Kusini kuwa ni kitisho. 

Wanadiplomasia wa China hata hivyo wamesema boti hizo zilikuwa zimetia nanga kutokana na kuchafuka kwa bahari, na hazikua na wapiganaji. Brunei, Malaysia, Ufilipino, Taiwan, China na Vietnam wamekuwa wakizozania eneo la bahari ya China Kusini, ambako biashara zenye thamani ya takriban dola trilioni 3.4 kwa mwaka hupitia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...