Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

Wanasheria wa Navalny kukata rufaa dhidi hukumu ya zaidi ya miaka mitatu jela

 


Wanasheriawa kiongozi wa upinzani Urusi, Alexei Navalny, wamesema watakata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miaka mitatu na nusu jela aliyohukumiwa mpinzani huyo.

Mahakama imesema Navalny alivunja sheria kwasababu hakuwa akiripoti katika mamlaka ya magereza kama ilivyotakiwa, wakati alipokuwa Ujerumani kwa matibabu baada ya kupewa sumu. Tangu mwaka 2014, Navalny amekuwa akikabiliwa na kesi ya madai ya udanganyifu iliyokuwa imesimamishwa kwa muda na ambayo amesema imechochewa kisiasa.

Kulingana na mawakili wake, huenda Navalny akatumikia kifungo cha miaka miwili na miezi minane kwa vile alishawahi pia kutumikia kifungo cha nyumbani siku za nyuma. Olga Mikhailova, ni mmoja wa mawakili wake:

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo na mahakama, Navalny alijitetea kwamba asingeweza kuripoti katika mamlaka ya magereza kama alivyotakiwa kisheria kwani alipoteza fahamu wakati akipelekwa Ujerumani kwa matibabu.

"Nilikuwa nikipatiwa matibabu Ujerumani," amesema Navalny akiwa mahakamani.

Lakini Jaji alisistiza kwamba alilazimika kutimiza masharti hayo katika hali yoyote ile.

"Mahakama imeamua kuunga mkono hoja ya Mamlaka ya Wafungwa," alisema jaji Natalya Repnikova wakati alitangaza uamuzi wa mahakama.

Na kwa mara nyingine mkosoaji huyo wa Rais Vladimir Putin amezishutumu mamlaka za Urusi kwa kujaribu kumuua kwa kumlisha sumu ya Novichok inayoathiri Neva.

Navalny alirudi Urusi kutoka Ujerumani mapema mwezi huu, licha ya kuonywa kwamba atakamatwa mara baada ya kuwasili nchini humo. Tangu alipokamatwa, Urusi imeshuhudia maandamano makubwa ya watu wengi katika wikiendi mbili tofauti pamoja na watu kadhaa kukamatwa na polisi.

Serikali ya Urusi sasa inataka kutuma wanajeshi kulinda mashule ili kuhakikisha wanafunzi hawashiriki katika maandamano hayo ya kumuunga mkono Navalny.

Mamalaka za Urusi zimekuwa zikijaribu kuzima maandamano hayo kwa njia yoyote iwezekanayo.

Na ndiyo maana zimeamua kuzilenga shule kwa vile waandamanaji wengi ni vijana wadogo.

Kulingana na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, vijana wa chini ya miaka 18 wapatao 205 walikamatwa kote Urusi katika maandamano ya Jumapili iliyopita.

Na maandamano zaidi yanatarajiwa kufanywa kufuatia hukumu hiyo ya mahakama dhidi ya Navalny.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...