Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

UWT Dodoma Mjini waadhimisha miaka 44 ya CCM kwa kugawa misaada kwa wenye uhitaji


KATIKA kuadhimisha miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini umekabidhi misaada yenye thamani ya Sh. Milioni Moja kwa watoto wenye ulemavu wa akili na kuwatembelea wakina mama waliojifungua katika Hospitali ya Mkoa.

Misada iliyotolewa ni pamoja na  Juisi, Mchele, Pipi, Sukari, Mafuta ya kupaka, Miswaki na Madaftari

Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Katibu wa UWT Wilaya ya  Dodoma Mjini, Diana Madukwa amesema wameamua kufanya  mambo yanayogusa jamii pamoja na kuwatembelea  ili kujua changamoto zinazowakabili  na kuyafikisha mahali panapohusika.

“Katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM tumeamua kwenda kutembelea watoto ambao wana ulemavu wa akili  na kuwapa msaada wakina mama ambao wamejifungua katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kwasababu ni maeneo  ambayo yanayogusa jamii moja kwa moja," Amesema Madukwa.

Madukwa ameiasa jamii  kuwa na tabia ya kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi na na wenye mahitaji maalumu huku akisisitiza jamii kuacha  tabia ya kuwanyanyapaa kundi hilo  kwani nao ni binadamu.

Amesema CCM ni chama tawala kinagusa kila tabaka na kuhakikisha kila mtu ambaye amezaliwa katika ardhi ya Tanzania anapata haki zake kulingana na maumbile yake.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...