Search This Blog

Monday, February 1, 2021

Umoja wa Ulaya walaani kukamatwa kwa waandamanaji Urusi


Mkuu wa sera ya kigeni ya Umoja wa Ulaya Josep Borrel amelaani vikali kukamtwa kwa waandamanaji na waandishi wa habari wa Urusi pamoja na utumiaji wa nguvu wa kupindukia unaofanywa na vikosi vya usalama nchini humo.

 Polisi imewakamata waandamanaji wapatao 4,400 kote nchini Urusi na kuufunga mji mzima wa Moscow ikiwa inajaribu kunyamazisha maandamano ya kudai kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny. 

Borrel amesema raia wa Urusi wana haki ya kuandamana bila hofu ya kukandamizwa na kwamba serikali ya Urusi inahitaji kufuata sheria za kimataifa. 

Borrel ameyasema hayo katika ziara yake ya siku tatu mjini Moscow, ambayo ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Umoja wa Ulaya tangu 2017.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...