Search This Blog

Monday, February 1, 2021

Maandamano mapya ya kumpinga Bolsonaro yafanyika Brazil


Mamia ya watu wameandamana tena jana kote nchini Brazil kupinga jinsi Rais Jair Bolsonaro alivyolishughulikia janga la virusi vya corona nchini humo. Wengi wanamtaka ajiuzulu au afunguliwe mashtaka ya kumuondoa madarakani. 

Katika mji wa Brasilia, watu wapatao 200 walishiriki katika maandamano hayo yaliyoitishwa na vyama vya mrengo wa kushoto. Maandamano sawa na hayo ya kumpinga Bolsonaro yalifanyika pia katika miji ya Sao Paulo na Rio de Janeiro. 

Ugonjwa wa COVID-19 umesababisha zaidi ya vifo 223,000 nchini Brazil. Baadhi ya wataalamu wanadai kwamba janga hilo limechochewa na aina mpya ya virusi vya corona iliyojitokeza hivi karibuni inavyosambaa kwa kasi zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...