Search This Blog

Monday, February 1, 2021

Chama cha Bobi Wine kupinga matokeo ya uchaguzi, mahakamani

 


Chama cha Bobi Wine kinasema wana ushaidi wa kutosha kuonyesha udaganyifu katika uchaguzi uliopita.Image caption: Chama cha Bobi Wine kinasema wana ushaidi wa kutosha kuonyesha udaganyifu katika uchaguzi uliopita.

Chama cha upinzani nchini Uganda cha NUP kinawasilisha leo Jumatatu, kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika Januari 14, 2021,.

Katika uchaguzi huo Rais Museveni aliibuka kuwa na ushindi kwa asilimia 58.38 huku mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi alipata asilimia 35.08.

Chama cha NUP kimethibitisha kwamba leo kinawakilisha kesi katika mahakama ya ya juu zaidi ya Uganda.

Idara ya mahakama imekanusha ripoti zilizokuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba mahakama ya juu imekataa kupokea kesi hiyo.

Makamu mwenyekiti wa chama cha NUP, John Batst Nambesh ambaye pia ni naibu mwenyekiti mkoa wa mashariki amesema wana ushaidi wa kutosha kuonesha udaganyifu uliofanyika katika uchaguzi uliopita.

Wagombea wengine wa Urais pia wamejitokeza kupinga wazi matokeo ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na Bw Patric Amuriat wa chama cha FDC, Jenerali Mugisha Muntu wa chama cha ANT, Norbert Mao wa chama DP na mgombea wa kujitegemea Jenerali Henery Tumukunde.

Jumla ya wagombea 11 walishiriki katika uchaguzi wa urais wa mwezi Januari ambapo Rais Museveni alitangazwa mshindi na kupata fursa ya kuendelea kuliongoza taifa la Uganda kwa muhula wa sita.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...