Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Serikali yapiga marufuku maandamano mapya Nigeria


Waziri wa Habari Lai Mohammed ameonya dhidi maandamano yaliyopangwa kufanyika huko Lekki jijini Lagos ambapo vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waaandamanaji mwezi Oktoba mwaka jana.

Maandamano mapya, yaliyopewa jina la 'Occupy Lekki toll gate', yamepangwa kufanywa Jumamosi Waandaaji wanasema watagomea dhidi ya kufunguliwa tena kwa lango la ushuru.

Bwana Mohammed amesema serikali haitaruhusu maandamano mengine kufanyika. Alisema wahalifu wanaweza kuvamia maandamano na kusababisha watu kupoteza maisha na uharibifu wa mali.

Amesema matangazo ya kuwataka watu kujitokeza kwenye maandamano yamekuwa yakisambazwa

Waziri aliongeza kuwa serikali ilikubaliana na matakwa ya awali na kuachiwa kwa waandamanaji waliokuwa wamekamatwa wakati wa wimbi la kwanza la maandamano na kuunda tume huru kutazama suala la ukatili wa polisi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...