Search This Blog

Friday, February 12, 2021

DC Tarime awaonya watakaovuja bilioni 2.-9 zilizotolewa na halmashauri


Na Timothy Itembe Mara                                                          

Mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri amehimiza halmashauri ya Tarime vijijini kutumia fedha iliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga minerais kwa ushirikiano na mgodi wa Barrick billion 2.09 kutumika katika maendeleo ya shuguli za kijamiii.

Akipokea fedha hizo kutoka kwa maneja mkuu wa mgodi wa Barrick ,Luiz Correia mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa serikali inamacho na fedha zinazotolewa kwaajili ya maendeleo ya wananchi kwa hali hiyo anaitaka halmashauri hiyo kutumia fedha hizo katika shuguli za maendeleo ya wananchi wala sio vinginevyo.

Mtemi aliongeza kusema fedha hizo ziende kujenga vyumba vya madarasa ili kuondoa uhaba uliopo,miundombinu ya barabara pamoja na kuboresha sekta ya  Afya kwa jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Meneja huyo alisema kuwa wanatarajia kuona matunda ya matumizi sahihi ya fedha hiyo katika kuboresha miundombinu ambayo inachangia kuimarisha uchumi na huduma mhimu kwa jamii.

Maneja huyo alifafanua kusema  kipimo cha mafanikio kwa kupitia mchango wa mgodi wa North Mara ni kuona matokeo endelevu yanayolenga kuimarisha huduma ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kwa jamii nzima.    

 “Kampu ni ya uchimbaji madini ya Twiga minerais a iliyoundwa kwa ushirikiano baina ya kampuni ya madini ya Barrick na serikali ya Tanzania kupitia mgodi wake wa dhahabu wa North Mara imekabidhi hundi yenye dhamani ya shilingi Bilioni 2.090,183,849 kwa halmashauri ya wilaya Tarime ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai hadi Desemba,2020”alisema Correia.

Correia alitumia nafasi hiyo kupongeza viongozi wa awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli pamoja na wananchi wanaozunguka migodi yote ya Barrick kwa ushirikiano na kudumisha Amani ambapo wanafanya shuguli zao kwa utulivu.

Maneja alimaliza kwa kusema kuwa wanapenda kuwapongeza viongozi wa serikali pamoja na wananchi kuanzia ngazi ya vijiji na kata ikiwemo halmashauri wanapochimba dhahabu kwa ushirikiano na juhudi wanazoziona za kusimamia vizuri matumizi ya fedha za ushuru ambazo zinalipwa kila  baada yamiezi sita,juhudi hizo zinatuhamasisha kufanya kazi zaidi na tulipe ushuru mkubwa na kuendelea kuchangia zaid maendeleo chanya katika wilaya Tarime vijijini na mkoa Mara kwa ujumla.

Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Simioni Kiles akipokea hundi hiyo kwa niaba ya madiwani wenzake na halmashauri kwa ujumla alisema kuwa fedha hiyo tayari zaidi ya shilingi milioni 400 wamezitengea bajeti ya kituo cha Afya kimoja ndani ya halmashauri hiyo,Matundu ya vyoo ndani ya shule sita na fedha zingine wataendelea kuzipangia bajeti kwa kuangalia masilahi mapana ya wananchi kadri vikao vitakapokuwa vinakaa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...