Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Mrithi wa Bensouda katika mahakama ya (ICC) kujulikana leo


Bi Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011Image caption: Bi Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011

Wajumbe wa nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wanakutana mjini New York baadaye leo kumchagua mwendesha mashita mpya wa mahakama hiyo.

Wagombea tisaikiwa ni pamoja na majaji wawili mmoja kutoka Nigeria na mmoja kutoka Uganda, wako katika orodha ya kumrithi Mgambia Bi Fatou Bensouda, ambaye muhula wake kama Mwendesha mashitakaMkuu wa mahakama hiyo unamalizika mwezi Juni mwaka huu.

Bi Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011- baada ya kuchukua nafasi ya wakili Muargentina Luis Moreno Ocampo.

Katika muhula wake madarakani, aliweza kuwatia hatiani washitakiwa Zaidi kuliko mtangulizi wake- na hivi karibuni ikiwa akiwa ni muasi wa zamani wa Uganda kamandaDominic Ongwen ambaye mwezi huu alipatikana na hatia za uhalifu wa kivita.

Hatahivyo alikabiliwa na ukosoaji mkubwa hususan ni kuhusu kesi zake kuwalenga Waafrika. Mwezi Juni mwaka jana, Bensouda alizuiwa kusafiri nchini Marekani wakati rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump aliposaini sheria ya rais inayoweka vikwazo vya fedha dhidi yake.

Watu wengine wanaowania nafasi ya Bensouda ni pamoja na:


1:Karim Khan- Wakili Kutoka


2. Robert Petit, Mwendesha mashitaka kutoka Canada


3.Susan Okalany- Jaji kutoka Uganda


4. Morris Anyah- Jaji kutoka


5. Fergal Gaynor - mwendesha mashitaka kutoka IRELAND


6. Fernandez Castresana- mwendesha mashitaka kutoka Uhispania


7. Francesco Lo Voi- mwendesha mashitaka kutoka Italia.


8. Brigitte Raynaud – mwendesha mashitaka kutoka Ufaransa


9. Richard Roy – wakili kutoka Canada



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...