Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema leo kuwa wanajeshi wa Eritrea walifanya mauaji ya kupanga dhidi ya raia wa Ethiopia wasio na silaha katika jimbo lililokumbwa na mzozo la Tigray.
Katika ripoti yake iliyochapishwa leo, Amnesty International imesema mauaji ya kutisha yalitokea kwenye mji wa kaskazini mwa Tigray wa Axum mnamo Novemba 28 na 29 mwaka uliopita ambapo wanajeshi walifyetua risasi mitaani na kufanya uvamizi wa nyumba kwa nyumba.
Manusura 41, mashahidi na watu wengine 20 wanaofahamu kilichotokea wamesema kulikuwa na mauaji, mashambulizi ya makombora na wizi mkubwa wa mali wakati vikosi vya Ethiopia na Eritrea vilipoendesha operesheni ya kijeshi na kuchukua udhibiti wa mji huo Novemba 19.
Licha ya Eritrea kukakusha kuhusika na mzozo wa jimbo la Tigray, shirika la Amnesty International limesema kiwango cha makosa yaliyotendeka kinatosha kuwa uhalifu dhidi ya binadamu

No comments:
Post a Comment