Search This Blog

Friday, February 26, 2021

Biden azungumza na mfalme Salman wa Saudi Arabia

Rais wa Marekani Joe Biden amezungumza kwa njia ya simu na mfalme Salman wa Saudi Arabia usiku wa kuamkia leo na kumweleza kuwa atafanya kazi ya kujenga mahusiano imara na ya uwazi baina ya mataifa hayo washirika. 

Kulingana na Ikulu ya Marekani, Biden na Mfalme Salman wamejadili kwa kirefu suala la usalama katika eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati na pia wamekumbusha kuhusu umuhimu wa uhusiano kati ya Washington na Riyadh.

 Mazungumzo kati ya viongozi hao yamefanyika wakati utawala wa Biden unatarajiwa kuchapisha leo ripoti ya siri iliyotayarishwa mwaka 2018 na mashirika ya ujasusi ya Marekani juu ya mauaji ya mwandishi habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi.

 Ripoti hiyo ni sehemu ya uchunguzi mpana unaofichua kuwa mtoto wa mfalme Salman ambaye ni mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed bin Salman aliidhinisha kuuwawa kwa Kashoggi nchini Uturuki, madai ambayo Saudi Arabia inakanusha.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...