Search This Blog

Friday, February 26, 2021

Côte d'Ivoire yakamata shehena kubwa ya dawa za kulevya


Vikosi vya usalama nchini Côte d'Ivoire vimekamata shehena yenye zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya cocaine wakati wa operesheni ya usiku kwenye mji mkuu wa taifa hilo la Afrika magharibi wa Abidjan. 

Polisi imesema dawa hizo za kulevya zimetokea nchini Paraguay na zina thamani ya dola za kimarekani milioni 46.7.

Janga la virusi vya corona limevuruga biashara haramu ya dawa za kulevya lakini vigogo wa biashara hiyo wanatumia mbinu za kusafirisha shehena kubwa ya dawa kwa kutumia meli zenye idadi ndogo ya mizigo pamoja na ndege za abiria.

Katika miaka ya karibuni shehena kubwa ya cocaine imekuwa ikipitishwa kwenye pwani ya Afrika Magharibi kutokea Amerika ya Kusini kuelekea barani Ulaya.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...