Aliyekuwa katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yenye makao yake makuu mjini Moshi, Arthur Shoo amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mkuu wa Dayosisi hiyo ambaye ndiye mkuu wa Kanisa hilo Tanzania, Askofu Fredrick Shoo amethibitishia Mwananchi Digital leo Februari 26, 2021 kuwa mtendaji wake huyo mkuu alifariki dunia jana usiku akiendelea na matibabu hospitali ya KCMC.
No comments:
Post a Comment