Search This Blog

Friday, February 26, 2021

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani aelezea hatua zinazochukuliwa za mchakato wa amani


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani alisema kuwa msingi mkubwa umeandaliwa kwa ajili ya amani nchini humo.

Akizungumza kwenye hafla aliyohudhuria katika mji mkuu wa Kabul, Ghani alibainisha kuwa ataendelea kushauriana na wabunge kuhusu suala la amani katika kipindi kijacho.

Akifahamisha kwamba Afghanistan iko katika hali nzuri zaidi ya kufikia amani ya kudumu na ya haki, Ghani alisema,

"Zaidi ya hapo awali, msingi mkubwa umeandaliwa kwa ajili ya amani nchini."

Rais Ghani alibaini kuwa fursa hii iliyopatikana inapaswa kutumiwa vyema.

Akielezea kwamba juhudi zinafanywa ili kuanzisha amani na kupata suluhisho nchini, Ghani aliangazia umuhimu wa kuharakisha mchakato wa amani.

Kwa upande mwingine, awamu ya pili ya mazungumzo kati ya Waafghanistan, ambayo ilianza Januari 6 katika mji mkuu wa Doha, nchini Qatar ili kumaliza vurugu zinazoendelea Afghanistan na kusitishwa baada ya wajumbe wa Taliban kuzuru nchi za kanda mnamo Januari 26, ilianzishwa tena tarehe 22 Februari.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...