Search This Blog

Friday, February 26, 2021

Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Waaswa kuyaishi maisha ya KAIZEN


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali watu wa wizara ya viwanda na biashara   Bi Veronica Nchango  amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kuishi maisha kwa kufuata misingi ya  Falsafa  ya KAIZEN  inayowahimiza  kuzingatia udhibiti wa mazingira ya kazi na kuboresha usimamizi wa raslimali kama vile Mda  Watu na Fedha  ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

Bi Nchango ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma kuanzia  Februari 23 hadi 25, 2021.  Pia Amewasisitiza watumishi hao kuzingatia ubunifu, ubora na tija ili kupunguza malalamiko, upotevu na gharama zisizokuwa za lazima katika utendaji kazi.

Amewahimiza watumishi hao kuwa chanzo cha mabadiliko katika utendaji wao na wawafundishe watumishi wenzao katika wizara nyingine pamoja na familia zao wakiwemo watoto wao ili wakue katika misingi ya kufanya kazi kwa ufanisi, tija na ubora nchini.

Aidha, Mkurugenzi huyo amewashauri wakufunzi wa Falsafa ya KAIZEN kuongeza S moja  inayomaanisha “Sensitization”  ili kuhamasisha watu zaidi kujifunza na kutekeleza falsafa hii katika kuongeza tija na ubora. “S” nyingine (5) tano  zinazotumika kama njia za utekelezaji wa KAIZEN ni Sasambua (Sort), Seti (Seti), Safisha (Shine), Sanifisha (Standardize) na Shikilia (Sustain).

Ameshauri mafunzo hayo yaliyolenga kuongeza ufahamu kuhusu falsafa KAIZEN inayolenga kuongeza thamani endelevu ya tija na ubora viwandani yaingizwe kwenye mitaala ya shule na yafundishwe nchi nzima ili kuhimili kufikia matokeo bora, makubwa na kwa haraka  na kuhimili ushindani

Aidha, Mkurugenzi huyo aliwapongeza watumishi hao kwa kuhudhuria mafunzo hayo pamoja na kutembelea Viwanda vinavyotekeleza falsafa ya KAIZEN vilivyopo jijini Dodoma kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo. Viwanda hivyo ni Dane Holding Limited kinachotengeneza mvinyo na kiwanda cha “Groly Farm” kinachozalisha mafuta ya Alizeti.

Utekelezaji wa KAIZEN nchini unayofadhiliwa JICA unalenga kuongeza tija na ubora katika sekta ya viwanda na shughuli za maisha ya kila siku inaongozwa na misingi ambayo ipo katika ubunifu wa mawazo, maarifa na ushiriki wa kila mtu ndani ya taasisi, shirika au kampuni ili kuhimili ushindani.

KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya badilika kwa ubora / uzuri linalohusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi mifumo michakato na nyanja yoyote ya kuendesha biashara. KAIZEN asili yake ni Japani lakini sasa inatekelezwa Duniani kote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...