Na Timothy Itembe Mara.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara,Elias Ntiruhungwa amekataa ombi la madiwani kutaka kununua gari la milioni 200 ambapo amesema kuwa halmashauri inaufinyu wa Bajeti.
"Kutokana na ufinyu wa Bajeti halmashauri yetu haitaweka bajeti ya kununua gari la shilingi milioni 200 hadi hapo tutakapopata ruhusa ya bajeti kutoka serikali kuu ndipo turidhie kununua"alisema Ntiruhungwa.
Bajeti kama ilivyopitishwa na madiwani tutaitekeleza na kuisimamia ili kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wetu aliongeza kusema Ntiruhungwa.
Hatua hiyo imekuja kutokana na diwani kata ya Nyandoto Fredy Sinfda Sabega kuhoji kuwa wanakubaliana na ushauri uliotolewa na Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki wa kununua Gari kwaajili ya halmashauri ambapo kuna uhaba wa magari.
Kwa upande wa madiwani walipitisha Bajeti ya shilingi bilioni 30.2 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwa ni pamoja na makusanyo ya vyanzo vya ndani,fedha ya ruzuku ya serikali pamoja na utekelezaji wa shuguli za maendeleo.
Zubeda Nkala mhazini wa halmashauri hiyo alisema kuwa makadirio na makusanyo ya mapato na matumnizi ya halmashauri Tarime Mjini kwa mwaka wa fedha 2021/2022 inaomba kuidhinishiwa kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 19,692,193,061.14 kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 1550000000.00 kutokana na vyanzo vya nadani,shilingi 814948000.00 kwa ajili ya ruzuku ya uendshaji (OC) na shilingi 14153009561.14 mishahara.
No comments:
Post a Comment