Rais wa Tanzania John Magufuli hii leo kuongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa katibu mkuu kiongozi John Kijazi.
Shughuli hiyo inafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Baada ya kuagwa kwa taratibu za kiserikali, mwili utasafirishwa hadi Korogwe mkoani Tanga ambapo atazikwa siku ya Jumamosi.
Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi amekuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 - 2016 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.
Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.

No comments:
Post a Comment