Search This Blog

Friday, February 19, 2021

Auhukumiwa kifo baada ya kumuua mtalii


Mwili wa mtalii huyo mwenye miaka 55-ulipatikana baada ya miezi kadhaaImage caption: Mwili wa mtalii huyo mwenye miaka 55-ulipatikana baada ya miezi kadhaa

Mahakama ya Algerian imemuhukumu mwanaume mmoja hukumu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtalii kutoka Ufaransa ,mwaka 2014.

Hervé Gourdel, 55, alitekwa nyara wakati akiwa anatalii katika mbuga ya taifa ya Djurdjura N. Picha video iliibuka ikionesha kifo cha mtalii huyo huku kundi la kigaidi la Jund al-Khilafa ambalo lina uhusiano na wanamgambo wa Kiislamu wa IS kudai kuhusika katika tukio hilo.

Mshukiwa mmoja, Abdelmalek Hamzaoui, alifika mahakamani Alhamisi huku wengine hawakufika. Hamzaoui alikanusha kuhusika katika mauaji hayo ,na kuiambia mahakama kuwa ameshutumiwa tu, kufunga kesi hii ni kuwafurahisha Wafaransa tu.

Waliokuwa na marehemu Gourdel wakati wa kupanda milima , walisema Hamzaoui ni miongoni mwa watekaji nyara. Licha ya hukumu hiyo ya kifo, Algeria ilisitisha kunyonga tangu mwaka 1993. Gourdel, alikuwa mpanda milima , alitembelea nchi hiyo wakati wa mapumziko na kuuliwa Septemba 2014.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...