Algeria inatarajiwa kuitisha uchaguzi wa mapema baada ya Rais Abdelmadjid Tebboune kulivunja bunge hapo jana Alhamisi.
Rais huyo wa Algeria katika taarifa yake amesema atafanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri. Ameeleza kuwa mabadiliko ni muhimu ili kuunda taasisi zinazoaminika.
Kiongozi huyo wa Algeria ameongeza kusema kuwa uchaguzi ujao lazima ufanyike bila dosari na kwamba anataka kuwaachilia huru wanaharakati walioko kizuizini.
Tamko hilo limetolewa muda mfupi kabla ya maadhimisho ya miaka ya miwili tangu kufanyika maandamano makubwa yaliyosababisha kuanguka kwa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Abdelaziz Bouteflika mnamo 2019.
Bunge lilichaguliwa mara ya mwisho mnamo 2017, wakati Bouteflika alikuwa na ushawishi na nguvu kubwa. Uchaguzi mpya haukutarajiwa nchini humo hadi mwaka ujao wa 2022.
Serikali ya Algeria imekuwa inakabiliwa na shinikizo katika siku za hivi karibuni. Waandamanaji wa eneola kaskazini mwa nchi hiyo wamekuwa wakidai demokrasia na kuitaka serikali iondoke madarakani.
Rais wa sasa Abdelmajid Tebboune alichaguliwa mnamo mwezi Desemba 2019. Wengi wa waandamanaji wanasema kiongozi huyo anahusiana na tabaka lililotawala shwa na nchi hiyo kwa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment