Search This Blog

Friday, February 19, 2021

Penzi la Harmonize na Kajala lanoga wachorana Tattoo kwenye shingo


Kwenye msimu huu wa makopakopa na malavidavi msanii na boss wa Konde Gang Music, Harmonize na mpenzi wake Kajala Masanja wamenogesha mahaba kwa kuchorana 'Tattoo' zenye herufi ya mwanzo ya majina yao.

Wawili hao wamechora Tattoo hizo kwenye shingo zao ambapo Harmonize ameandika herufi ya jina la Kajala kwa maana ya 'K' na mpenzi wake Kajala  Masanja naye ameandika herufi 'H'.

Kwa sasa penzi la Harmonize na Kajala ndiyo linazungumziwa zaidi kwenye habari za kiburudani na siku ya Valentine walienda Visiwani Zanzibar kula bata, pia msanii Harmonize amemtungia wimbo wa kumsifia mpenzi wake huyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...