Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kwamba watu wengine wawili wameambukizwa virusi vya homa ya Ebola.
Waziri wa Afya wa jimbo la Butembo, Eugene Nzangu Salita amesema mmoja kati ya watu hao aliambukizwa mbali na kitovu cha mlipuko.
Watu hao walikumbwa na maambukizi kwenye miji iliyopo umbali wa kilometa 150 kutoka magharibi ya mji huo wa Butembo ambako maambukizi mengine yalizuka.
Mpaka sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kwamba watu sita wamepatikana na virusi vya homa ya Ebola na watu wawili wameshakufa tangu kulipuka tena kwa maradhi hayo katika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa Februari.
No comments:
Post a Comment