Search This Blog

Friday, February 19, 2021

Ethiopia yaishutumu Sudan kuchochea ghasia mpakani


Serikali ya Ethiopia imeishutumu Sudan kuchochea mgogoro kati ya mataifa mawili ambayo yamekuwa katika mvutano kutokana na mzozo wa mpaka.

Ghasia ziliibuka mwishoni mwa mwaka jana kuhusu eneo la wakulima wa Ethiopia ambao Sudan wanasema waliingia katika eneo lao.

Pande zote mbili zimekuwa zikishutumiana kwa kusababisha ghasia.

Mvutano umekuja wakati Ethiopia ikiwa na mgogoro kaskazini mwa ukanda wa Tigray.

Katika taarifa kali iliyotolewa na serikali ya Ethiopia , imelishutumu jeshi la Sudan kuchochea mvutano huo kuingia kwenye vita.

Licha ya kudai mzozo huu kuhusiana mvutano w eneo la wafugaji walioko karibu na mpaka lakini inaonekana wazi masuala ya kisiasa kuhusika pia.

Taarifa ya Ethiopia imesema jeshi la Sudan linachochea mgogoro ili kuinufaisha Misri.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Ethiopia na serikali ya Misri juu ya ujenzi wa bwawa katika mto Nile.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...