Search This Blog

Friday, February 19, 2021

Uingereza na Canada zawawekea vikwazo majenerali wa Myanmar


Uingereza na Canada zimeongeza shinikizo dhidi ya majenerali wa Myanmar kwa kuwawekea vikwazo ingawa majenerali hao hawaonyeshi dalili yoyote ya kuondokana na mbinu za kutumia nguvu na kuwaweka watu kizuizini katika juhudi zao za kukandamiza upinzani dhidi ya mapinduzi waliyofanya nchini humo. 

Hata hivyo kiongozi wa vijana wa mapinduzi ya kijeshi ya Myanmar na mwanaharakati Thinzar Shunlei Yi amesema wamefurahishwa na vikwazo hivyo vipya kutoka Uingereza na Canada.

 Amesema waandamanaji wanajiandaa kuingia barabarani leo Ijumaa siku ambayo itatimia wiki mbili tangu kuanza maandamano ya kila siku katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa Aung San Suu Kyi ambaye sasa anazuiliwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...