Search This Blog

Wednesday, February 10, 2021

Naibu Waziri Kigahe akutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi Dodoma


Na.Ezekiel Mtonyole - Dodoma

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika leo tarehe 9 Februari 2021 jijini Dodoma Mhe Kigahe  aliwaagiza kuwasilisha changamoto walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Mhe. Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Aidha, Mhe.Kigahe amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa.

Aidha amesema kuwa amekuwa wakianda  na kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 – 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 – 2032.





No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...