Search This Blog

Wednesday, February 10, 2021

DCC Manispaa ya Tabora yapitisha mapendekezo ya bajeti ya bilioni 50.7 kwa mwaka ujao wa fedha


KAMATI ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) imepitisha mapendekezo ya makisio ya kukusanya shilingi bilioni 50.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa  2021/22.

Akiwasilisha jana katika Kikao maalumu cha DCC, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema makusanyo yajayo yatatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 45.6 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na Halmashauri imelenga kukusanya shilingi bilioni 5 ni fedha kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani .

Nduguru alisema kwa upande wa makusanyo ya mapato ya ndani wamelenga kuongeza asilimia tano ya makusanya ya ndani kutoka ya shilingi bilioni 4.8 za mwaka wa 2020/21 hadi bilioni 5 ya mwaka ujao wa fedha wa 2021/22.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha wamepanga kutumia shilingi bilioni 7.6 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Nduguru alivitaja vipaumbele katika bajeti ijayo ni ujenzi wa Stendi kuu yenye eneo la ukubwa wa Hekari 50 katika Kijiji cha Inala , ujenzi wa soko la kisasa, ukarabati wa machinjio, uendelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, uboreshaji wa miundombinu ya elimu , soko kuu na barabara za Manispaa na ukarabati wa ukumbi wa sanamu ya Mwalimu Nyerere.

Alisema katika mwaka wa fedha unaondelea wa 2020/21 walikisia kukusanya na kutumia shilingi bilioni 43.8 kutoka vyanzo mbalimbali.

Nduguru alisema hadi kufikia Desemba ,2020 walikuwa wamekusanya bilioni 15,6 sawa asilimia 36 ya bajeti iliyopitishwa



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...