Search This Blog

Wednesday, February 10, 2021

KMC FC yatia timu Rukwa, kamili kuvaana na Tanzania Prisons

 


TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, Jana, Februari 9 alfajiri ilisepa  jijini Dar es Salaam kuelekea Mkoani Rukwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa siku ya Ijumaa saa 8.00 mchana katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Kikosi hicho cha wana Kino Boys kimewasili salama kikiwa na wachezaji 20, viongozi watano pamoja na benchi la ufundi.

Ni mara ya kwanza kwa KMC FC  kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Nelson Mandela. 

 KMC ipo Rukwa ikiwa imetoka kucheza mechi yake ya kiporo dhidi ya Namungo na kuweza kuibuka na  ushindi wa mabao 3-0  ina alama 25 huku ikiwa kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imeshacheza michezo 18 hadi sasa.

 Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kupata pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

"Tupo tayari na kila mchezaji ana morali ya kufanya vizuri ndani ya uwanja, hakuna majeruhi hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," .



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...