Search This Blog

Tuesday, February 9, 2021

Mzazi mbaroni kwa kugoma kuandikisha watoto shule

 


Merchades Mugishagwe mkazi wa manispaa ya Bukoba Mkoa wa Kagera amekamatwa na polisi kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo akidaiwa kukaidi agizo  la kuwaandikisha watoto wake watatu shule.


Wakati mzazi huyo akiishia mikononi mwa polisi, watoto akiwemo mwenye umri wa miaka 13 wameandikishwa na jana Jumatatu Februari 8, 2021 walianza kwenda shule.


Watoto wengine wa familia hiyo walioandikishwa na kuanza masomo katika shule ya msingi Buyekera manispaa ya Bukoba wana umri wa miaka tisa na mitano.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buyekela, Jacob Kaijage amesema mtoto mkubwa mwenye umri wa miaka 13 ameandikishwa darasa la nne, mwenye umri wa miaka tisa ameandikishwa darasa la pili huku mdogo mwenye umri wa miaka mitano ameandikishwa darasa la awali.


Watoto hao wamepelekwa shule chini ya ulinzi wa usimamizi wa maofisa wa halmashauri wa manispaa ya Bukoba baada ya uongozi wa Serikali Wilaya ya Bukoba kuingilia kati uamuzi wa wazazi wao wa kutowapeleka shule kutokana na imani yao ya dini.


Ofisa elimu Manispaa ya Bukoba, Elipidius Baganda ndio aliyesimamia shughuli ya kuwanunulia sare na vifaa na mahitaji yote kabla ya kuwapeleka shule watoto hao kutokana na fedha zilizotolewa na ofisi ya mbunge wa Bukoba, Steven Bwabato.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...